Kaunti ya Trans nzoia inajivunia uwanja wa maonyesho ya kilimo Kwa miaka sitini na Saba ambao sasa ni wa jadi na umewasaidia wakulima kupata fursa ya kujifunza maswala ya kilimo. Uwanja huu wa maonyesho ukiwa mojawapo ya maeneo yaliyojengwa enzi za mkoloni.
Uwanja huo ulianzishwa na serikali ya wakoloni mwaka wa 1956 ambao ulitokana na eneo hilo kuwa na ardhi yenye rotba. Iliwapa wakoloni tamaa ya kuelezea katika eneo hili ambalo liliwasaidia kukutana na kujifunza mengi kuhusu kilimo. Na baada ya mkoloni kuondoka wakenya waliendeleza tamaduni ya kuandaa maonyesho ya kilimo kila mwaka katika eneo hili.
Onyesho hili limeonekana kuwa mojawapo ya maonyesho ya zamani na bado lipo hadi sasa huku wengine wakibuni kutoka Kwa hilo na wakulima kukariri kuwa mabadiliko ya tabia nchi yanawakosesha usingizi.
Wakulima hawa wanahaja ya kujua mbinu za kisasa za kusalia kwenye kilimo huku wakishauriwa kwenda kupokea masomo wenyewe badala ya kutuma watoto wao; haswa wakulima wa maharagwe na mahindi .
Pia serikali inatakiwa kushinikiza idara mbalimbali ili kutumia fursa ya maonyesho ya kilimo kufunza Umma huduma zinazotoa.
NA FAITH MISANYA