Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ni miongoni mwa mawakili chini ya chama cha AIMI MA LUKENYA,chama hicho kimefika na kuwasilisha ombi mahakamani likitaka ubomoaji wa nyumba unaoendelea Mavoko kaunti ya Machakos kusitishwa,jaji anayesikiliza kesi hiyo katika mahakama ya mazingira Annet Nyakuri alimpa kinara huyo wa Wiper kuwasilisha hoja zao mbele ya mahakama hiyo.
Kwa sasa wakaazi wa eneo hilo la mavoko katika Kaunti ya Machakos wameachwa bila makao kufuatia ubomoaji unaoendelea ,wakaazi hao wamefurushwa kwenye ardhi hiyo yenye utata inayodaiwa kumilikiwa na kampuni ya AFRICAN PORTLAND CEMENT.Kalonzo amelalamikia jinsi shughuli ya ubomozi inavyokiuka haki za kibinadamu.
Wakaazi wa eneo la Mavoko wanamtaka rais William Ruto kuamuru ubomoaji huo kusitishwa,wakaazi hao wameitaka serikali kutekeleza haki kwa usawa wakisema kwamba pia wao ni wananchi wa taifa hili,licha ya ubomozi huo kuendelea katika eneo hilo wakaazi hao wamesema wapo tayari kununua ardhi kwa njia halali.
Hapo jana mbunge wa Mavoko Patrick Makau, alihojiwa na idara ya upelelezi nchini DCI kwa mda wa saa mbili kuhusu utata wa ardhi huko Mavoko,inadaiwa mbunge huyo ni miongoni mwa watu wengine 29 ambao wanadaiwa kuchunguzwa na idara ya upelelezi kuhusu utata wa ardhi.
Walioathirika na ubomozi ni wafanyibiashara, wamiliki hoteli, wanafunzi, waumini wa madhehebu mbalimbali na wananchi.
Na Felix Wanjala