kushindwa kwa baraza hilo la usalama kuingilia kati kwa mara ya kwanza hadharani katika mgogoro wa Israel na Gaza kulifuatia kukataliwa kwa rasimu iliyoungwa mkono na urusi siku ya juma tatu.
wakati wajumbe 12 kati ya 15 wa baraza hilo wamepiga kura kuunga mkono azimio lililoongozwa na Brazil kwenye kikao kuhusu mzozo wa mashariki ya kati, mjumbe mmoja ambaye ni Marekani amepiga kura ya kuyapinga, na wawili ambao ni Urusi na uingereza hawakupiga kura.
ikumbukwe kura ya ‘Hapana’ kutoka kwa yeyote kati ya wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo la usalama inasimamisha hatua yoyote iliyowekwa mbele ya baraza hilo , wanachama wa kudumu wa baraza la usalama ni Uchina, Ufaransa,Shirikisho la Urusi, Uingereza na Marekani.
Kabla ya kura hiyo, marekebisho mawili yaliyopedekezwa na Urusi yakitaka kusitishwa kwa mapigano mara moja , ambayo ni ya kudumu na kamili, na kusitisha mashabulizi dhidi ya raia yalikataliwa na baraza la usalama.
Balozi wa Urusi Vassily Nebenzia alisema ” wakati wa mafumbo ya kidiplomasia umepita zamani .yeyote ambaye hakuunga mkono rasimu ya azimio la Urusi kuhusu suala hili atawajibika kwa kile kinachotokea.
Alisema marekebisho ya Urusi yalipendekeza mwito wakukomesha mashambulizi ya kiholela dhidi ya raia na miundombinu huko Gaza.
Na Samuel Ngoya