Meneja wa Bodi ya NCPB Tawi la Bungoma, Samuel Waitara, amekanusha vikali madai ya ufisadi katika
shughuli ya kupeana mbolea kwa wakulima, akizungumza na waandishi wa habari ofisini mwake.
Waitara amesisitiza kuwa shughuli hiyo inafuata utaratibu na masharti yaliyowekwa na serikali.
Madai ya ufisadi yalizuka baada ya Mbunge wa eneo bunge la Kanduyi, John Makali, kutoa taarifa
kwenye sherehe za Mashujaa, akidai kuwa Waitara anaficha mbolea na kuuzia madalali. Waitara
amejitolea kushirikiana na viongozi wa eneo hilo ili kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu utaratibu wa kuuzia
wakulima mbolea ya serikali.
Wakulima wa eneo hili wamegawanyika kuhusu shughuli hii. Baadhi yao wana wasiwasi kuhusu
upatikanaji wa mbolea kwa bei nafuu, huku wengine wakionyesha imani kwa utaratibu uliopo. Hali hii
inaonyesha umuhimu wa kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini ukweli kuhusu shughuli hii ya kununua
mbolea ya serikali.
na Abigaely Wanjala