Elizabeth Kisiangani |
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Nzoia kaunti ya Bungoma amerai asasi za serikali kuweka usalama wa watahiniwa wa Gredi ya 6 na wale wa darasa la 8 wakati wanapojiandaa Kuanza mtihani wao wa kitaifa wiki lijalo.
Katika mahojiano baada ya sherehe za kutoa maombi kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Nzoia,mwalimu mkuu wa shule hiyo Lydia Namisi amesikitika kwa kosa lililofanyika kaunti ya Baringo kilichowaacha wanafunzi kuwa na hofu baada ya shule ya Kapindasum na kambi ya GSU kuvamiwa.
Shule hiyo ilifunguliwa mwaka huu Januari baada ya kufungwa mwaka wa 2012 kutokana na matukio ya ujambazi katika maeneo haya huku oparesheni ya kukomesha uhalifu ilifanikisha kufunguliwa kwa shule hiyo.
Aidha,Bi Namisi alichukuwa fursa hio kuwahimiza wazazi kuwa makini na watoto wanapofunga kwa likizo ndefu ili kupunguza utovu wa nidhamu kule nyumbani.
Hata hivyo,mtihani wa kitaifa wa KCPE na ule wa gredi ya 6 unatarajiwa kuanza rasmi wiki lijalo siku ya jumatatu na utatakiwa kumalizika siku ya Jumatano tarehe 1 Novemba.