

ROYAL BLOOD EPISODE 2.MONDAY TO FRIDAY Tunaendeleza kipindi chetu Cha kifilipino huku tukimpata Buana Napoy Terrazo kwenye ofisi mkuu pamoja na Gustavo Royales(Babake Napoy). Napoy anamwambia Gustavo kuwa mana yake ambaye ni Betty aliishi akimwambia kwamba baba yake alishakufa. Napoy hakuwahi amini ya kwamba alikuwa na baba.Napoy anamuuliza Gustavo kuwa yeye ni nani:Tunaonyeshwa kumbukumbu miaka mingi iliyopita huku ambavyo Gustavo alimwacha mamake Napoy wakati aligundua kwamba mamake Napoy (Betty)ni mjamzito.
Gustavo anamdanganya Napoy na kusema kuwa alikuwa busy saba kazini na pia ilichangia kuachana na Betty.Gustavo anamjulisha Napoy kwamba mamake(Betty) alidhania kuwa Gustavo alikuwa na mwanamke mwingine.Napoy ananwambia Gustavo kuwa kwa Sasa yupo zaidi ya miaka 30 na haiwezekani kwamba Gustavo alikuwa akimtafuta.Gustavo anamwambia Napoy kwamba hatanii kabisaa.
Gustavo anaamua kumsaidia Napoy kwenye upasuaji wa bintiye Lizzy. Napoy na Gustavo wanaamua kufanya vipimo vya DNA Ili kugundua kama Napoy ni mwanawe Halisi wa damu.Napoy haamini kabisa,Je,Nini mwisho wa Stories ya Napoy? Tutakuja kujua hapo mbeleni.Rafiki yake Napoy kutoka Kijijini(Otep) anamwambia Napoy kwamba mama mkwe alikuwa anamtafuta kule Kijijini. Kiasi hiviiii,,Lizzy(Bintiye Napoy) anashikwa na maumivu makali sana Tena tumboni. Napoy anamkimbiza hospitalini.Kwa Bahati mzuri Daktari anamwambia kwamba bintiye Yuko sawa na atapona haraka. Anajulishwa kuwa Buana Gustavo Royales atashughulikia malipo na gharama ya hospitalini yote.Napoy aombwa kupeana sampuli yake ya DNA.
Gustavo afisini nwake anafuta kazi mshirika wake mmoja kwa ukali mkubwa sana. Pale hospitalini tunampata Napoy na mwanawe wakiwa pamoja kwenye family times ๐.Mamake mkwe msumbufu anampigia simu Napoy na kumuuliza kwa Nini hataki kumpatia mjukuu wake. Wanagombana kwenye simu.Lizzy anamwambia baba yake Napoy kwamba ajaribu kuelewana na bibi.Upande mwingine Nako mambo yanachemka!Mamake mkwe wa Napoy anapanga kufungua kesi dhidi ya Napoy Ili ampate mjukuu wake. Yaani ndo Napoy ametoka tu kwa shida huko Kijijini Sasa sai amepata utajiri alafu huyuu mama yake mkwe hamtakii aki jamani binadamu Hawa,sisemi kitu Mimi!
Ghafla bin vuu,Gustavo anaingia chumbani hospitalini na kumwambia Lizzy kwamba wataenda kuishi pamoja kwa sababu DNA imeonyesha kwamba Napoy ni mwanawe Halisi wa damu wa Gustavo Royales. Sasa Napoy (Dingdong Dantes) ni mmoja wa The Royales Great Family. Napoy amwambia Gustavo kuwa mama yake (Betty) angekuwa hai kama Gustavo angekuwepo wakati huo.

MWENDELEZO…Napoy anamshukuru Gustavo kwa kumsaidia kwenye gharama ya mwanawe hospitalini. Sasa wameelewana na Napoy anamsamehe na kumkubali Gustavo Kama baba yake mzazi.Napoy anawaaga marafiki zake Kijijini na kutoka na Gustavo kuelekea kuishi na Gustavo Royales in the Royales Mansion. Sasha anamwambia Napoy kuwa wataongea kuhusu hisia zao baadae. Kumbe Sasha anampenda Napoy na hataki kusema.Tuko Sasa kwa The Royales baada ya Napoy na bintiye Lizzy kuletwa huko. Babu Gustavo (Tirso Cruz รญรญรญ) anawaambia kuwa wasiambie mtu kuwa yeye ni mtoto wake. Alafu hii compound ya Royales family ni kubwaa alafu its very beautiful.
Gustavo Ako na familia na watoto wake ikiwemo Beatrice, Kristoff na Margret.Margret kwa umbali anaonekana akiwasorora akina Napoy huku akiomba sala ya Mungu.Anakaa mpoolee hivi alafu anakaa pia mwenye roho mbayaaaa..acha tungojeee huku mbeleni tuone Margret Binti wa Gustavo alivyo! Wakati wa chakula Napoy na mwanawe Lizzy wanafurahia kwelikweli.Huku Gustavo hajawaambia wanawe kwamba Napoy ni mmoja wa wanawe. Nawaambia hii italeta shida kubwaa. Follow Senรตr Wabwile kwa updates za Kila siku.Gustavo anamwambia Napoy kuwa yeye Sasa ni mwanawe rasmi na hastahili kufanya kazi yoyote ile.
Gustavo anampatia Napoy kazi kwenye kampuni yake ya Royal Motors. Napoy na bintiye wanapatiwa vyumba vyao vya kupendeza sana. Hii ni nzuri saaaanaaa. Napoy anamuuliza Bi Chloe(Mjakazi) jinsi Buana Gustavo anavyowayendea huku akisema kuwa Buana Gustavo ni mwema sana. Je,ni ukweli kuwa Gustavo ni mwema?Napoy na mwanawe Lizzy wanapelekwa matembezi na yule mfanyakazi. Lizzy anaanza kumfuata yule mbwa wa nyumbani huku akielekea kwenye barabara.Karibu mtoto wa watu akufeee. Karibu gari la Beatrice (Binti ya Gustavo) limgonge Lizzy.
Upande mwingine Gustavo anasikika akiongea na jamaa wake stori fulani Kali sana kuhusu uchunguzi.Je,ni Siri Gani ambayo Gustavo anaweza kuwa nayo?Tutakuja kujua hapo mbeleni nitakapowaambia kila kitu. Beatrice hata hajali kama anamgonga mtoto mchanga na gari lake la kifahari. Napoy ndiye aliyekimbia na kumwokoa bintiye.The last 5 minutes nawaachia mumalizie mkienjoy venye Binti ya Gustavo Ako na nyoka mkubwa sana akisema kwamba huyo nyoka ni mtoto wake.Kinachoonekana ni kwamba Familia ya Royales sio mzuri hata kidogo. Vita vitachipuka kwenye familia hii wakati Napoy atakavyotambulishwa.Je,maoni yako ni yepi kuhusu kipindi hiki kipya Cha โRoyal Blood โ kwenye runinga ya mwananchi ya Tandao TV?