

Mashindano ya Gofu ya Magical Kenya Open 2025 yameingia siku ya pili kwenye uga wa gofu wa Muthaiga, yakiwa na washiriki 156 kutoka sehemu mbalimbali. Tukio hili lilianza rasmi Alhamisi huku mchezaji bingwa, Darius van Driels, akilenga kutetea taji lake. Katika duru ya kwanza, Mwingereza John Parry aliibuka kinara, huku wachezaji wa Kenya wakishuhudia matokeo duni na kuonekana chini kwenye orodha ya viongozi.Wakenya hawajafanya vizuri katika mtokeo yaliyopita, na hakuna Mkenya aliyewahi kushinda mashindano haya katika historia.

Hali ya wachezaji wa Kenya ni ya mshike mshike, baadhi yao walichujwa jana huku wengine wakiendelea na awamu ya pili leo. Benjamin Herbert alikuwa akiongoza baada ya kikao cha asubuhi kwa 13 chini ya par, akifuatiwa na John Parry aliyechukua uongozi kwa 8 chini ya par 63 siku ya kwanza. Blomstrand alikuwa na 8 chini ya par, Gouveia Ricardo 7 chini ya par, na Jayden Schaper 7 chini ya par 64.Licha ya matokeo haya, wachezaji wa Kenya hawakukata tamaa, wakisema kuwa hawajapata mazoezi ya kutosha lakini bado wana nia ya kufanya vizuri.