

By Felix Wanjala.
Hivi Ndivyo hali ivyokuwa katika hafla ya mazishi ya mbunge Charles Were,yaliyofanyika eneo la kachieni eneo bunge la Kasipul kaunti ya Homabay.
Wabunge wa mrengo wa serikali,walimtaka kiongozi wa ODM Raila Odinga kufanya mazungumzo na baadhi ya viongozi wanachama wa ODM, kukumbatia ushirikiano wake na rais William Ruto.
Aidha wito wa heshima miongoni mwa vyama hivyo viwili,pia ulishamiri kwenye mazishi hayo.Mawaziri wanachama wa ODM,walimtaka katibu mkuu wa chama Edwin Sifuna,kukoma kuwasuta kutokana na msimamo wao kuhusu serikali wanayoihudumia,sifuna aliwakosoa mawaziri hao kwa madai kwamba wanahujumu utendakazi wake ndani ya chama.

Spika wa bunge la kitaifa aliyewasilisha ujumbe wake kwa familia ya mwendazake.Aliwataka baadhi ya viongozi wachanga kutoka ODM kuunga mkono ushirikiano wa rais William Ruto na kinara wao Raila Odinga.
Kwa upande wake kinara wa ODM Raila Odinga anasema kuwa chama cha ODM kidemokrasia na kila mmoja ana haki ya kutoa maoni yake. Ila ametaka viongozi kutoa maoni hayo kwa heshima.