

By Felix Wanjala.
Gavana wa kaunti ya Transnzoia George Natembeya, ameibuka tena na kuanza kuikosoa serikali ya rais William Ruto. Kiongozi huyo amesema eneo la magharibi linahitaji kiongozi mpya atakaewasilisha maslahi ya wakaazi katika meza ya kitaifa.
Kwenye kaunti za vihiga, Kakamega,na viunga vyake,alihubiri wito wa umoja miongoni mwa wakaazi,kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027.pia aliikashifu serikali kwa madai ya kutumia raslmali za eneo hilo, kunufaisha watu binafsi.
Alipotua kaunti ya Bungoma,Natembeya aliahidi kukomboa eneo la magharibi, kutoka mikononi mwa viongozi, aliodai wanatumia eneo hilo kwa manufaa yao binafsi,aliwataka viongozi wakuu kutoka eneo hilo, wakiongozwa na Spika wa bunge la kitaifa Moses wetangula, na mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi,kuwaeleza wakaazi wa eneo hilo, kuhusu manufaa ya mkataba waliotia saini, kati yao na serikali ya Kenya kwanza.
Huku kampeni ya kusaka uungwaji mkono miongoni mwa viongozi ikiendelea,baadhi wanadai eneo la magharibi lina nafasi nzuri ya kumteua kiongozi, atakaeongoza taifa,ikizingatiwa kuwa eneo hilo ni la pili kwa idadi kubwa ya kura, baada ya eneo la mlima Kenya.Natembeya amekuwa mkosoaji mkuu si tu wa serikali ya kitaifa, bali ameibuka kuwa kiongozi anayepania kutwaa usukani wa kuongoza jamii pana ya mulembe.baadhi ya wananchi walitoa kauli zao kuhusu jinsi mawimbi ya kisiasa,yanaendelea kuvuma eneo hilo.