
ELDORET, KENYA - MAY 20: Jonathan Kitum, age 16, with a friend during a computer class at Kipkeino Highschool. He is a promising long distance runner and he has already trained for an hour from 5.15 in the morning.

By Felix Wanjala.
Baraza la Mitihani la Kitaifa Nchini Kenya (KNEC) limetangaza tarehe ya mwisho kwa mitihani ya mwisho ya baadhi ya kozi zilizopitwa na wakati katika elimu ya kiufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET).
Kupitia barua iliyowasilishwa kwa wakuu wa taasisi hizo, KNEC imesema mitihani ya mwisho kwa kozi hizi zisizo za mfumo wa moduli itafanyika Novemba 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa KNEC, Dkt. David Njengere, amesisitiza kuwa taasisi zinazotoa kozi hizi ambazo zimeshaanza kuondolewa hazitaruhusiwa kuandikisha wanafunzi wapya baada ya mitihani ya Novemba 2025.
Baraza limeeleza kuwa limewapa muda wa kutosha taasisi husika kufanya mabadiliko na kuhamia katika mtaala mpya wa moduli uliotayarishwa na Taasisi ya Kitaifa ya Kuendeleza Mitaala (KICD).
Hata hivyo, licha ya miongozo hiyo kuwa wazi, baadhi ya taasisi bado zinaendelea kuandikisha wanafunzi wapya kwenye programu zilizopitwa na wakati, kwa kisingizio cha kuwahudumia wanafunzi waliokuwa na mitihani ya marudio.
Daktari Njengere ameonya kuwa tabia kama hiyo ni kinyume na maadili ya elimu na inahatarisha uaminifu wa mfumo wa elimu nchini.Kozi zinazofutwa ni pamoja na programu mbalimbali za kiufundi na biashara.
Baadhi ya hizo zitabadilishwa na kuingizwa katika mtaala mpya, huku zingine zikiondolewa kabisa.Kozi kadhaa za kiufundi na biashara zimeorodheshwa kufutwa katika mabadiliko ya hivi karibuni yanayoendeshwa na Baraza la Mitihani la Kitaifa (KNEC).
Miongoni mwa kozi zinazolengwa ni: Stashahada ya Ufundi (Craft Certificate) ya Uhandisi wa Mitambo,Uhandisi wa Magari,uchomeleaji wa Vyuma ( welding) Ufundi wa Umeme, na vifaa vya Kielektroniki pamoja na Utambuzi wa Hitilafu.
Kulingana na KNEC, baadhi ya kozi hizi zitaingizwa katika mtaala mpya ulioboreshwa, huku zingine zikiondolewa kabisa.
Baraza pia limebainisha kuwa baadhi ya programu hizo zilifutwa baada ya kushindwa kuvutia watahiniwa wa kutosha.Hata hivyo, KNEC imeweka wazi kuwa imekuwa ikitoa nafasi maalum kwa wanafunzi waliokuwa na mitihani ya marudio (referrals) katika kozi zilizoondolewa, ili waweze kukamilisha masomo yao.
Licha ya hilo, baadhi ya taasisi zimetumia mwanya huo kuandikisha wanafunzi wapya katika programu zilizokamilisha muda wake, bila sababu za wazi.
Baadhi ya kozi zilizoboreshwa na kubadilishwa majina ili kuendana na mahitaji ya sasa ya sekta mbalimbali Ni Stashahada ya Teknolojia ya Habari (Diploma in Information Technology – 2209 sasa imeboreshwa na kuchukua nambari mpya 2910.
Stashahada ya Baiolojia Tumia (Diploma in Applied Biology – 230) sasa inapatikana chini ya msimbo mpya 2914,Stashahada ya Usimamizi wa Lishe (Diploma in Dietetics Management – 2406) imebadilishwa kuwa 2916,Cheti cha Ufundi katika Teknolojia ya Maabara ya Sayansi (Craft Certificate in Science Laboratory Technology – 1408) sasa kinapatikana kwa nambari 1904,Cheti cha Ufundi katika Teknolojia ya Uvuvi (Craft Certificate in Fishery Technology – 1409) sasa kinatambulika kwa msimbo 1908.