
Trucks carrying sugar cane on a road in Kenya.

By Felix Wanjala.
Wakulima wa miwa sasa wana sababu ya kutabasamu baada ya serikali kupitia Wizara ya Kilimo kuelekeza baadhi ya kampuni za sukari kuongeza bei ya ununuzi wa zao hilo.
Kwa mujibu wa agizo hilo, bei ya tani moja ya miwa imeongezwa kutoka shilingi 5,300 hadi shilingi 5,500 — ongezeko la shilingi 200 kwa kila tani.Katika barua rasmi iliyotiwa saini na Katibu wa Wizara ya Kilimo, Dkt. Kiprono Rono, kampuni zitakazonufaika na ongezeko hili ni pamoja na Muhoroni, Mumias, kampuni ya sukari ya Naitiri, Olepito na Brooke.

Akizungumza jana wakati wa mkutano na viongozi kutoka kaunti za Machakos, Kitui na Makueni, Rais William Ruto alieleza kuwa mageuzi yanayoendelea katika sekta ya kilimo yanalenga kumuinua mkulima wa kawaida.
Aidha, Rais Ruto aliahidi kuwa wakulima wa kahawa na chai huenda nao wakaona mafanikio mwezi ujao wa Juni, huku serikali ikiweka mikakati ya kuhakikisha wanalipwa kwa wakati pindi wanapowasilisha mazao yao kwa kampuni husika.