

FELIX WANJALA.
Polisi kwa ushirikiano na maafisa wa NACADA,wamenasa washukiwa kumi wa Bangi na pombe haramu katika eneo la shinyalu na ikolomani katika kaunti ya Kakamega.
Bangi ya thamani ya shilingi milioni 1.5,lita 3000 ya pombe haramu aina ya chang’aa na lita 100,000 ya kangara iliharibiwa. Afisa mtendaji wa NACADA akitoa onyo kwa waraibu wote msako bado unaendelea.
Ametoa wito kwa wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya Kushughulikia maswala muhimu yanayohusu ujenzi wa taifa.
takwimu muhimu kutoka kwa Ripoti ya Kitaifa ya Nacada ya mwaka 2022, kuhusu matumizi ya pombe na dawa za kulevya katika eneo la Magharibi,inayojumuisha kaunti kama Bungoma, Kakamega, Busia, Vihiga, na Trans Nzoia. Inaongesha kuwa.
Eneo la Magharibi lina viwango vya juu vya matumizi ya pombe, takribani 23.8% ya watu wenye umri wa miaka 15โ65 wanaotumia pombe.
Kaunti za magharibi zinangoza kwa kiwango cha matumizi ya changโaa (pombe haramu) kwa 11.4%.
Huku pombe ya kiasili kama vile busaa yakiwa katika 12.9%
Eneo Hilo pia linaongoza kwa idadi ya watumiaji wa dawa mbalimbali kwa jumla: 26.4% ya watu wa eneo hilo wanatumia angalau aina moja ya dawa au pombe.