

Baadhi ya wananchi wameelezea wasiwasi wao kuhusu tabia ya viongozi kuanza kampeni za kisiasa mapema, wakisema hali hiyo inakwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kote nchini.
Wananchi hao wanatoa wito kwa viongozi kuacha siasa za mapema na badala yake kuelekeza nguvu zao katika kuboresha huduma muhimu kama elimu, afya, usalama na uchumi maeneo wanayosema yanawaathiri kwa kiasi kikubwa.Hata hivyo, kuna wengine wanaoona tofauti. Baadhi ya wananchi wameonekana kuunga mkono kampeni za mapema, wakidai kuwa hali hiyo imewapa nafasi ya kuwasiliana moja kwa moja na viongozi na kufaidika na rasilimali zinazotumika katika shughuli hizo.
Zikiwa zimesalia takriban miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027, baadhi ya viongozi tayari wameanza kuonyesha nia ya kugombea nyadhifa mbalimbali, hali inayoashiria mchuano mkali wa kisiasa unaojijenga mapema.