Criminologist behind the barricade tape, working at the crime scene in abandoned warehouse, taking a blood sample from the floor with a cotton swab

BY FELIX WANJALA
Mali yenye thamani kubwa imeharibiwa baada ya kundi la vijana kudaiwa kuvamia kituo cha burudani kinachomilikiwa na Mbunge wa Kabuchai, Mheshimiwa Majimbo Kalasinga, eneo la Musese.Tukio hilo linadaiwa kuwa na misingi ya kisiasa, likihusishwa na uchaguzi mdogo wa Chwele–Kabuchai unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa wafanyakazi wa hoteli hiyo, vijana hao walishambulia majira ya mchana, wakivunja madirisha na kupora vinywaji kama vile pombe pamoja na fedha taslimu.
Meneja wa hoteli hiyo, Geoffrey Kitutu, amesema washambuliaji hao walionekana kulenga kuhujumu biashara hiyo, akiripoti hasara inayokadiriwa kufikia mamilioni ya pesa.Anatoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa haraka na kuwakamata waliohusika.Mke wa Mbunge huyo, Bi. Janet Majimbo, amelaani vikali tukio hilo, akizitaka idara za usalama kuongeza ulinzi kwa familia yao, akidai kuwa kundi hilo hilo lilitoa vitisho vya kuvamia makazi yao.
Wakazi wa eneo hilo wameelezea wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama, wakisema tahari za kisiasa kabla ya uchaguzi mdogo zimezidisha hali ya hofu katika jamii.