Akizungumza Nakuru kwenye na viongozi wa KNUT wa eneo la bonde la ufa,katibu wa muungano wa walimu KNUT Collins Oyuu alionya tume ya mitihani ya kitaifa
nchini KNEC dhidi ya kuchelewesha malipo ya walimu watakaosimamia mitihani ya KCSE, KCPE na KAPSEA.
Oyuu alizidi kuonya huku akitishia kuongoza walimu kwa migomo iwapo tabia hii itaendelea . Alizidi kusema kuwa wameshuhudia utepetevu huu kila wakati ,hata hivyo mwaka huu wa 2023 wanatumai utofauti ambapo malipo kwa walimu kuzingatiwa kwa wakati ufaao.
Kando na kutolipwa na wakati mwafaka kwa walimu wanaosimia na kusahihisha mitihani hukumbana na changamoto kama udanganyifu wa mitihani, uhaba wa rasilimali za kutosha, upangaji wa masomo kwa njia za mitaala , uvujaji wa mitihani na uhaba wa muda wa kusahihisha maelefu ya karatasi za mitihani.
Abigaely Wanjala