Faith Misanya
Vijana 4,500 wanaohitimu NYS sasa wataweza kujiunga na idara ya polisi mwaka ujao pamoja na shirika la huduma kwa wanyama pori, KWS kuanzia mwezi ujao.
Hivi karibuni itawalazimu wale wanaotazamia kujiunga na kazi za utumishi wa Umma na vikosi vya ulinzi na usalama kuwa na vyeti vya kuhitimu kutoka Kwa chuo cha mafunzo Kwa vijana cha taifa ,NYS.
Waziri wa utumishi Moses Kuria ametangaza kuwa hivi karibuni wafanyikazi Watakao pania kujiunga katika kazi za utumishi wa Umma watahitajika kuwa na mafunzo na vyeti kutoka shirika la NYS akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kuiuhisha taasisi ya NYS katika ziara yake ya Kwanza chuoni humo.
Kuria amesema vijana 4,500 ambao wamehitimu watatarajiwa kupata kazi katika idara ya polisi na shirika la KWS kuanzia mwezi ujao na itawalazimu wale wanaotazamia kujiunga na kazi ya utumishi wa Umma kuhitimu kutoka kwa chuo cha mafunzo Kwa vijana cha taifa ,NYS.
Chini ya mpango uliozinduliwa taasisi ya NYS itakuwa na ongezeko la kila mwaka la usajili wa vijana hadi idadi ifike elfu laki moja mwaka wa 2027.