
BY FELIX WANJALA
Baadhi ya wahudumu kutoka kituo Cha kuegesha magari mjini Bungoma,wameitaka wizara ya biashara chini ya Afisa mkuu Douglas Sasita,kutoa ratiba ya chaguzi katika kituo hicho,kama vile ilivyofanyika katika soko kubwa wiki chache zilizopita.
Wahudumu Hawa walizungumza wakiwa nje ya afisi ya wizara ya biashara mjini Bungoma,walionyesha ghadhabu yao kwa wizara hiyo kwa madai ya kuzembea kazini.Wamemtaka Gavana Kenneth Lusaka,Seneta wa Bungoma Wafula wakoli na Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula kuingilia kati ili kutatua swala Hilo kabla ya mda kuyoyoma.Huku rais William Ruto akiendelea na ziara ya maendeleo eneo Hilo wahudumu hao wametishia kuwasilisha malalamishi yao Moja kwa Moja kwenye hafla atakayohudhuria rais William Ruto.
Mambo halipoonekana kuchacha afisa wa Biashara Douglas Sasita,alifika kwa haraka afisi mwake ili kutuliza hali.Afisa huyo mkuu alifichua kuwa alikuwa akihudhuria mkutano wa rais Ruto katika maeneobunge ya mlima Elgon, eneo bunge la Sirisia na katika soko la chwele eneobunge la kabuchai,kabla ya kupokea simu kuwa Kuna wageni fisini mwake,waliotaka majibu kuhusu uchaguzi wa kituo Cha kuegesha magari mjini Bungoma.
Aliwataka wahudumu hao kuwa watulivu huku akifichua kuwa atashauriana na mwanasheria mkuu wa Kaunti kuhusu utata u nalozingira swala zima la uchaguzi, wahudumu hao wametakiwa kufika Tena afisini mwake jumatano ya wiki ijayo ili kupata ufafanuzi zaidi.