
BY FELIX WANJALA
Ziara ya maendeleo ya rais William Ruto,katika eneo la Magharibi imegeuka na kuwa uwanja wa majibizano,kejeli na siasa za matusi baina ya viongozi wakuu nchini. Rais ametumia hatua hiyo kuwashambulia viongozi wa upinzani aliodai ni wao walianzisha siasa za matusi kuhusu maisha binafsi ya mtu.
Rais William Ruto Leo akiwa katika Kaunti ya Busia,ameendeleza kauli zake za kejeli dhidi ya baadhi ya viongozi,ametilia shaka jinsi wanavyokula na kuhusu namna wanavyoweza kushiriki mazoezi ya akusaidia miili yao.
Viongozi wa upinzani pia hapo wameonekana kukerwa na jinsi rais anaendesha siasa zake pia wakiamua kujibu kwa matusi. Wanadai afisi ya rais yafaa iheshimiwe na Kila mmoja anayeshikilia wadhifa huo.Kando na jinsi viongozi hao wanavyokula chakula rais aliwasuta baadhi yao kwa kukosa kuoa,na kwamba hawawezi kamwe kuruhusiwa kuongoza Taifa hili.
Ila Mwanasiasa anayedaiwa kulengwa hii Leo alimtambulisha mkewe hadharani na kusisitiza kuwa Yuko kwenye ndoa. Hivyo baadhi ya wakaazi wanadai eneo la Magharibi limeonekana kutumiwa kuwa uwanja wa majibizano wanamtaka rais kuzingatia swala la uzinduzi wa maendeleo pasi na kuendesha siasa za matusi.