
BY FELIX WANJALA
Mkataba wa ajenda kumi uliotiwa Saini na kiongozi wa UDA rais William Ruto na mwenzake wa ODM Hayati Raila Odinga, unaendelea kuibua hisia,licha ya Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna kudai kuwa mda wa maelewano ya mkataba huo ulitamatika machine 7.
Rais William Ruto akiwa katika eneo la kapsabet Kaunti ya Nandi Katika ziara ya maendeleo ametumia fursa hiyo kuwasuta anaodai wanapinga ushirikiano wa ODM na UDA kuwa wanalemaza utekelezaji wa makataba huo.
Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna alipuzilia mbali mkutano wa kiongozi wa chama Oburu Oginga na rais William Ruto katika jumba la KICC waliojadili ushirikiano kati ya ODM na UDA,Sifuna anadai ni waliangazia maswala yanayowahusu wao binafsi na Wala si wakenya.
Baadhi ya wananchi wanadai dkt Oburu Oginga amemsaliti aliyekuwa Kinara wa ODM Hayati Raila Odinga kwa kushiriki mazungumzo bila kuzingatia maslahi ya wanachama.Wanadai watazingatia mwelekeo wa Katibu wa chama kuhusu mstakabali wa ODM kuhusu ajenda kumi zinazojadiliwa.Baadhi wamedai ufisadi ndio chanzo Cha mgogoro baina ya viongozi vijana na wale wazoevu wamemtaka rais kupigana na ufisadi kwa manufaa ya maendeleo.