Operesheni ya usiku wa manane Trans Nzoia imeacha wakazi na maswali mengi baada ya polisi kuvamia makazi kumtafuta Desmond Shivachi.
BY SIMIYU VIONA

Operesheni ya usiku wa manane Trans Nzoia imeacha wakazi na maswali mengi baada ya polisi kuvamia makazi kumtafuta Desmond Shivachi.
Maafisa wa usalama walifanya msako mkali kwa saa kadhaa kuanzia usiku hadi alfajiri. Walifunga barabara, wakafanya upekuzi nyumba kwa nyumba, na milio ya magari ya polisi ilitawala eneo hilo. Wakazi wengi walilazimika kubaki ndani kwa hofu.Shivachi baadaye alijisalimisha kwa polisi na sasa anaendelea kuhuiliwa na maafisa wa DCI kwa uchunguzi zaidi.
Hata hivyo, wakazi wamelalamikia namna operesheni ilivyofanyika. Bor alisema walishtushwa na magari mengi yaliyofika ghafla usiku. Boaz akaongeza kuwa watoto waliogopa sana na wengi walikesha nje.
Wakili Karani amekosoa matumizi ya nguvu, akitaka sheria ifuatwe wakati wa operesheni kama hizo. Gavana Natembeya pia amesisitiza kuwa usalama ni muhimu, lakini haki na utu wa wananchi lazima ziheshimiwe.
Polisi bado hawajafanua sababu kamili ya msako huo. Viongozi wa eneo hilo wamewaomba wakazi kudumisha utulivu wakati uchunguzi ukiendelea.