Kwa mara nyingine kaunti ya kakamega iligonga vyombo vya habari kufuatia kisa kingine cha wanafunzi wa shule ya upili ya Eregi,kuugua maradhi yasiyojulikana huku ikibainika kuwa baadhi yao walikosa maji ya kutosha mwilini na baadae kushindwa kutembea na kupooza.
Zaidi ya wanafunzi 90 wamelazwa katika hospitali tofauti tofauti kutokana na maradhi hayo tatanishi,ambapo wanafunzi 30 wamelazwa katika hospitali ya kakamega level 5,31 katika hospitali ya mukumu,14 shibwe level 4 na wengine ishirini katika Iguhu level 4.
Wanafunzi walioathiriwa zaidi,wengi wao wamo katika kidato cha kwanza hadi cha tatu ambapo 48 wa kidato cha kwanza,39 kid a to cha pili,15 kidato cha tatu na 1 akiwa katika kidato cha nne. Waziri wa afya kaunti ya kakamega alithibitisha kwa kusema kuwa,sampuli za waathiriwa zilipelekwa katika maabara ya KEMRI kwa uchunguzi ambapo kwa sasa umebainiwa kuwa ni ugonjwa wa Mass Hysteria.
Happy Jumatano,wazazi waliwasili katika shule hiyo ili kuweza kuwachukua wanao ambapo walipata ruhusa kutoka kwa mkuu wa afya pamoja na walimu na hii ilikua baada ya maamuzi kufanywa. Kulingana na waziri wa elimu Ezekiel Machogu,alisema kuws wanafunzi watatakiwa kurejea shuleni siku ya jumatatu wiki lijalo,baada ya hatua muhimu kuchukuliwa ili kuzuia kujirudia kwa hali kama hiyo.