Rais wa marekani Joe Biden anatarajiwa kuzuru israel,hapo kesho, kuthibitisha kujitolea kwa marekani kwa usalama wa israel. Hayo yakijiri miito inaongezeka kwa israel kufungua njia, ilikuruhusu misaada kuingia Gaza.
Ziara hiyo ya rais wa marekani, Biden nchini Israel, imetangazwa na waziri wa mambo ya nje wa marekani Antony blinken leo jumanne.
Blinken amesema rais Biden atathibitisha tena uungwaji mkono thabiti wa marekani kwa israel na kujitolea kwa marekani kwa usalama wa israel.
Blinken ameongoza kuwa Israel ina haki na mujibu wa kuwalinda raia wake dhidi ya Hamas na makundi mengine ya kigaidi na kuzuia mashambulizi ya siku za usoni.
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kukutana na Blinken waziri wa ulinzi wa Israel Yoav Gallant alisema “Hivi vitakuwa vita vya muda mrefu , gharama itakuwa kubwa. lakini tutashinda kwa ajili ya Israeli na Wayahudi na kwa maadili ambayo nchi zote mbili (Israeli na Marekani) zinaamini”.
Na Samuel Ngoya