Kiongozi wa nupinzani nchini Raila Odinga pamoja na viongozi wengine wamezuiwa hii leo kushuhudia ubomozi wa nyumba unaoendelea eneo la Mavoko kaunti ya Machakos,siku chache zilizopita serikali ilitoa amri ya kubomolewa kwa nyumba hizo baada ya kudaiwa kujengwa katika ardhi inayomilikiwa na kampuni ya East Africa Portland Cement.
Majumba ya kifahari ikiwemo hoteli,shule,nyumba za watu binafsi,makanisa pamoja na misikiti ilibomolewa,majibazano makali baina ya mkuu wa polisi anaendesha oparesheni hiyo ya ubomozi na viongozi wa upinzani yalishuhudia eneo hilo.
Odinga amehutubia wakenya akiwa Mavoko kaunti ya Machakos, kiongozi huyo wa upinzani nchini amesema serikali ya Rais williamu Ruto imefeli kuwatumikia wakenya jinsi ilivyoahidi katika kampeni za uchaguzi wa mwaka jana,aidha ameitaka serikali kuchunga mali ya wananchi na haki zao za msingi.
Swala la gharama ya maisha lilichipuka hapa, Osinga anasikitishwa na jinsi sarafu ya taifa la kenya inaendelea kushuka huku wakenya wakibebeshwa mzigo mzito wa kulipa ushuru.
Felix Wanjala