Shirika la msalaba mwekundu limethibitisha mateka wawili wameachiliwabhuru na kundi la hamas na limewasafirishwa nje ya ukanda wa Gaza , kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu imesema imesimamia kuwachiwa huru kwa mateka hao na kwamba liko tayari kuendelea kufanya jukumu hilo katika siku za usoni.
Katika taarifa yake iliyotolewa hapo kabla , kundi la hamas lilisema limewaachia huru wafungwa wawili wanawake kwa sababu za kibinadamu, wanawake hao walioachiliwa na kundi hilo wamekabidhiwa kwa jeshi la Israel na wamepelekwa katika kituo cha afya nchini Israel .Kwa mujibu wa taarifa ya afisi ya waziri mkuu wa Israel wanawake hao ni Nurit cooper, mwenye umri wa miaka 79 na yocheve lifshitz wa umri wa miaka 85.
Israel imetaka kuachiliwa huru bila masharti mateka wote wanaoshikiliwa na kundi la Hamas ambalo linaorodheshwa kama la kigaidi na Israel, Umoja wa Ulaya , Marekani na mataifa mengine ya magharibi.
Jeshi la Israel lilisema jana kwamba watu wapatao 222 wakiwemo wa Israeli, raia wa kigeni watoto na wanawake walitekwa nyara na kupelekwa Gaza.
Na Samuel Ngoya