Asilimia kubwa ya misitu katika kaunti ya Homa-Bay imeharibiwa kwa kuteketezwa na hata baadhi ya misitu hii ikanyakuliwa.Hata hivyo,juhudi zaidi zimeanza kufanywa kupitia shule kuhakikisha misitu inalindwa.
Katika shule ya Msingi na shule ya upili ya Oriu eneo bunge la Karachonywo ambapo shughuli ya upanzi wa miti zaidi ya elf moja unaendelea huku wanafunzi wakishikilia mstari wa mbele.Lengo kuu ni kuwahimiza kutunza mazingira na kuboresha misitu.
Visa vya kuteketeza misitu hasua katika eneo la ngwanzi vimekuwa vikiwakosesha usingizi wana maeneo hawa huku hofu Tao kuu ikiwa ni uangamizaji WA miti ya kiasili ambayo ina umuhimu kama tiba katika jamii.
Wito sasa ulitolewa kwa washika dau mbalimbali kupiga cheki wanamazingira hawa ili kuboresha mazingira na kuhifadhi misitu ambayo kwa sasa imeadhirika pakubwa.
na Faith Misanya