Baada ya kupata mazao yasiyoridhisha, wakulima kutoka Kaunti ya SIAYA wamegeukia ukulima wa nanasi.
Joseph Agunda ni miongoni mwa wakulima waliopata hasara kutokana na upanzi wa mahindi. Pia, amesema Kuwa kinyume na ukulima wa mahindi, mananasi yanaleta faida Kwa miaka mingi.
Agunda alipanda miche elfu sita ya MANANASI ambayo Kwa sasa shamba lake Lina zaidi ya MANANASI elfu thelathini, hata hivyo, pia amesema Kuwa mananasi yanahitaji kuondolewa magugu kila mwezi ambayo imekuwa na gharama ya juu zaidi.
Agunda pia amesema Kuwa anaepuka gharama ya kupalilia shamba kila mwezi Kwa kutandaza migomba ya ndizi baina ya mimea ili kuzuia Kuota Kwa magugu .
Na Magret Ongwala