Faith Misanya
fadhili ulipokezwa kiasi cha pesa shilingi milioni 9.9 katika Kaunti ya Kisumu kutoka ubalozi wa Uholanzi ili kuanza mchakato wa kuboresha vijito katika Kaunti hiyo.
Ufadhili huo,utaendesha miradi kama vile upanzi wa miti,kutoa mafunzo Kwa wakazi,kuzoa majitaka pamoja na kuweka miundomsingi ya kusambaza maji Safi.
Serikali ya Kaunti ya Kisumu imepokea ufadili wa shilingi milioni 9.9 itakayotumiwa kwa upanzi wa miti huku dunia ikikabiliana na mabadiliko ya tabia nchi .Mito katika Kaunti hii hazijasazwa huku kiwango cha maji katika mto Kiboski kupungua maradufu na kuwaathiri wakazi zaidi ya laki mbili katika eneo Bunge la Kisumu magharibi.
Fedha hizi zinasemekana kuwa zimepeanwa kwa kutumiwa kurejesha Hali ya mto Kiboski na vijito vingine vya maji vilivyo adhiriwa na ukosefu wa Mvua.
Kando na Hilo pia fedha hizo zitatumiwa katika mchakato wa kubuni sheria za kulinda vyanzo vya maji ili kuzuia uharibifu wa mazingira .Kadhalika,kaunti ya Nakuru na Laikipia zitapokea shilingi milioni 13 na shilingi milioni 10 mtawalia ili kufadhili miradi ya utunzi wa maji.