

Brigid Sikuku.
Viongozi wa chama cha Ford Kenya katika eneo bunge la Kabuchai wamekutana kujadili mwelekeo wa kisiasa na maandalizi ya mchujo kuelekea uchaguzi mdogo wa wadi ya Chwele.
Hii ni baada ya mmoja wa waliokuwa wagombea, DCC Eric Wanyonyi, kutangaza kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho ili kuunga mkono mshikamano ndani ya chamaKatika taarifa yake DCC Erick Wanyonyi alitangaza kwa heshima na uwazi kuwa hatawania tena kiti cha MCA katika wadi ya Chwele, akieleza kuwa uamuzi wake umetokana na nia ya dhati ya kuhakikisha mshikamano ndani ya chama na mafanikio ya Ford Kenya katika uchaguzi huo.
“Nimejiondoa katika uchaguzi wa Chwele Kabuchai ambao utafanyika Septemba 27”
Uamuzi huo umepokelewa kwa mikono miwili na viongozi wa chama hicho, wakiongozwa na mwenyekiti wa Ford Kenya katika eneo la Kabuchai, Mheshimiwa Polycarp Wandabusi, ambaye amempongeza Wanyonyi kwa kile alichokitaja kama uamuzi wa kishujaa unaoweka mbele maslahi ya chama na wananchi.”Ningependa kupongeza uamuzi wa ndugu yetu Erick Wanyonyi,ni mfano wa uongozi wa kweli.”Wandabusi alisisitiza kuwa Ford Kenya itaendesha mchujo wake kwa njia
-
Kinyang’anyiro cha ugavana Bungoma.
Share this postFELIX WANJALA Mchakato wa kuwania kiti cha ugavana katika Kaunti ya Bungoma unaendelea kushika kasi huku
-
Bungoma County Workers Threaten Protests Over Permanent Contracts.
Share this postFLORENCE SIMIYU The Bungoma County Workers’ Union has issued a stern warning to the county government,
-
Ford Kenya Yaimarisha Mshikamano Kabuchai Kufuatia Kujiondoa kwa Wanyonyi.
Share this postBrigid Sikuku. Viongozi wa chama cha Ford Kenya katika eneo bunge la Kabuchai wamekutana kujadili mwelekeo
huru na ya haki, bila upendeleo, ili kumpata mgombea bora atakayepeperusha bendera ya chama hicho kwa kuzingatia maadili, uadilifu na uwezo wa kuhudumia wananchiKwa upande wake, Mkurugenzi wa uchaguzi wa chama hicho, Bi. Khadija Mustapha, aliwahimiza wanachama kujitokeza kwa wingi na kushiriki mchakato huo kwa amani, nidhamu na kuheshimu maamuzi ya chama ili kudumisha mshikamano.
Bi Khadija aliongeza kuwa maandalizi ya mchujo huo yako katika hatua za mwisho, huku kamati ya uchaguzi ikiwahakikishia wanachama wote kuwa kila kura itahesabiwa na sauti ya mwanachama yeyote haitapotea.Katibu wa Ford Kenya katika eneo hilo, Bw. David Milimo, alibainisha kuwa chama hicho kimejipanga kuendeleza kampeni za Amani Na wazi huku kikijitahidi kushughulikia malalamiko yoyote kwa njia ya haki na haraka.
Viongozi hao kwa pamoja walisisitiza kuwa uchaguzi huo ni fursa ya Ford Kenya kuonyesha umoja na nguvu yake katika siasa za mashinani, hasa kwa kuzingatia kuwa Kabuchai ni mojawapo ya ngome muhimu za chama hicho.Kwa sasa macho yote yako kwa Ford Kenya na mchujo wao unaotarajiwa kuvuta hisia si tu za wafuasi wa chama hicho, bali pia za wadau wote wa kisiasa katika kaunti ya Bungoma. Ni wazi kuwa chama hicho kimeweka msingi imara kuelekea uchaguzi mdogo wa wadi ya Chwele.