
NAIVASHA, KENYA - 2025/03/20: Kenyan President William Ruto addresses Kenyans during the official flag-off ceremony held at KICC. Safari Rally Kenya held in Kenya was held from 20th - 23rd March 2025. It is known as one of the toughest and most unpredictable events on the calendar, it challenges drivers with rough terrain, deep ruts, and the ever-present threat of sudden rainfall. Set in the heart of Kenya's breathtaking landscapes. The event was based in Naivasha in the Nakuru County, and consisted of twenty-one special stages, covering a total competitive distance of 384.86 km (239.14 miles).. (Photo by Boniface Muthoni/SOPA Images/LightRocket via Getty Images)

BY FELIX WANJALA.
Baadhi ya wakaazi wameelezea matumaini yao kuwa Rais William Ruto atatekeleza ahadi aliyoitoa hivi karibuni ya kuchangia kwenye bima mpya ya afya ya SHA, ili kusaidia Wakenya wasiokuwa na uwezo kumudu huduma za afya.
Wakizungumza na wanahabari, wakaazi hao waliongeza kuwa mchango wa viongozi wakuu, wakiwemo wabunge na magavana, utakuwa mfano bora wa uongozi wa kuwajali wananchi wa kawaida.Aidha, wananchi wengine wamepongeza hatua zinazochukuliwa na serikali kukabiliana na vitendo vya ufisadi katika sekta ya afya. Wanatumaini kuwa juhudi hizo zitaimarisha uwajibikaji na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Wakati huo huo, baadhi ya wananchi wamewataka Wakenya kumruhusu Rais Ruto kuendelea kutekeleza ajenda yake, wakisema bado ana takribani miaka miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa 2027 – muda wanaoamini unatosha kuona mabadiliko chanya.Katika kikao na viongozi wa kaunti ya Turkana, Rais Ruto alitangaza kuwa atachangia wakenya1.5 kwa ajili ya bima ya afya, na akatoa wito kwa wabunge na magavana kuungana naye kwa kuchangia kwa hiari ili kuwasaidia maelfu ya Wakenya wasiojiweza.