
BY FELIX WANJALA
Ziara ya rais William Ruto kwenye Kaunti za kakamega, Bungoma na Busia imekosolewa na baadhi ya wananchi wanaomtaka rais kukoma kutumia eneo la Magharibi,kuwatusi wapinzani wake wakisema hatua hiyo inadhalilisha jamii ya Mulembe.
Wananchi hao wanamtaka rais kushughulikia swala la afya Bora kwa wakenya,elimu,Kilimo,ajira,usalama na kupigana na ufisadi.Wananchi hao walitoa hisia mseto kuhusu hatua ya baadhi ya mashirika ya kutetea haki za binadamu kuwataka wabunge kuwasilisha mswada bungeni ya kumwondoa rais mamlakani.
Baadhi wanadai kumwaondoa rais mamlakani wakati huu utakuwa ni kupoteza tu mda,wametoa wito wa wananchi na viongozi wa upinzani kuwa watulivu na kujiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao.Matamshi ya viongozi hao wakuu yamevutia hisia mseto nchini baada ya kuanza kuoandisha joto la kisiasa wamewataka viongozi hao kuangazia matamshi yao yasije yakazua taharuki nchini.
Siasa zinazoendelea nchini kwa Sasa zimeonekana kuwa zenye matusi ukilinganisha na za hapo awali.Rais William Ruto aliahidi ujenzi wa uwanja wa kisasa katika Kaunti ya Busia,alizindua ujenzi wa soko mjini cheptais,soko linaloendelea la chwele na soko jipya la amagoro pamoja na uzinduzi wa jumba la huduma center, Kimilili na mradi wa smart city eneo la uwanja ndege Kaunti ya Bungoma miongoni mwa miradi mwingine.