
BY FELIX WANJALA
Chama Cha ODM kinaendelea kukumbwa na changamoto ya uongozi huku kukizuka makundi hasimu yanayotaka kuwepo mageuzi ya; ni nani yafaa awe Kinara baada ya kifo Cha Hayati Raila Odinga.
Baadhi ya wananchi wametoa wito kwa uongozi wa chama hicho kuwepo mazungumzo ya kina ili kutatua tofauti miongoni mwao.Licha ya hayo mbunge wa Embakasi mashariki Babu Owino, amesisitiza kuwa ni lazima kiongozi wa chama Oburu Oginga aitishe mkutano wa NDC ili kufanya mageuzi ya uongozi.Kauli ya viongozi Hawa imedaiwa kuwa inahatarisha umoja wa ODM na hivyo huenda pia kikasambaratika kama vyama vingine katika siku za usoni.
Aidha baadhi ya viongozi wanaonekana kuhusisha changamoto zinazokabili ODM na chama tawala Cha UDA,wanadai serikali imo mbioni kulemaza shughuli za chama hicho katika siasa za humu nchini.
Kiongozi wa chama Oburu Oginga, amesisitiza kuwa ataendelea kudumisha umoja wa wanachama na kwamba hakuna yeyote atakayetimuliwa ndani ya ODM.