Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta na Naibu Rais wa Zamani Rigathi Gachagua wakati wa ibada ya mazishi ya aliyekuwa Seneta wa Kirinyaga Daniel Karaba, Kaunti ya Kirinyaga, Aprili 1, 2026.
BY FELIX WANJALA

Kwa mara ya kwanza tangu kampeni za uchaguzi mkuu wa 2022, Rais mstaafu Uhuru Kenyatta na Naibu Rais wa zamani Rigathi Gachagua wamekutana jukwaa moja katika mazishi ya aliyekuwa Seneta wa Kirinyaga, Daniel Karaba.
Katika hotuba yake, Kenyatta alitoa wito kwa viongozi kushirikiana kwa manufaa ya maendeleo ya taifa, akisisitiza umuhimu wa mshikamano wa kisiasa. Gachagua, ambaye wakati wa kampeni za 2022 alimkosoa vikali bosi wake wa zamani, safari hii alionekana kumtaka Rais William Ruto kuacha kuingilia uhusiano wake mpya na Kenyatta.
Tofauti za kisiasa baina ya wawili hao ziliibua mjadala mpana, huku viongozi wa upinzani wakihimiza maridhiano na mshikamano, wakidai kuwa mshirikiano wao unaweza kuwa nguzo ya kuondoa uongozi wa Rais Ruto, wanaodai unawakandamiza wananchi.
Tukio hili limeibua taswira mpya ya siasa za Kenya, likionyesha uwezekano wa muungano wa kisiasa usiotarajiwa kuelekea uchaguzi wa 2027.