Magari mawili ya huduma ya matibabu ya dharura barabarani. Mtazamo wa kuchagua juu ya flasher kwenye paa la ambulensi. Mandhari uokoaji, uharaka na huduma ya afya.
SYPHROSE NAFULA

Ajali ya Mti Tongaren.
Kijiji cha Kahawa Lumukile, eneo bunge la Tongaren, Bungoma, kimegubikwa na simanzi baada ya kijana mwenye umri wa miaka 20 kufariki kwa ajali ya mti ulioporomoka na kumuangukia wakati wa shughuli ya ukataji.
Kwa mujibu wa familia, marehemu alikuwa akifanya kazi ya kukata mti mkubwa kabla ya kuangukiwa ghafla, na majeraha aliyopata yakawa chanzo cha kifo chake. Emily Munialo, jamaa wa karibu, alieleza kuwa familia imepoteza kijana mwenye bidii na tegemeo kubwa nyumbani.
Wakazi wa kijiji wameeleza masikitiko yao, wakisema tukio hilo limeacha pengo kubwa na kuibua hofu kuhusu usalama wakati wa shughuli za ukataji miti.
Chifu wa Mbakalo, Melissa Estock, ametoa wito kwa wananchi kuwa waangalifu na kutumia vifaa vya usalama, akisisitiza umuhimu wa kushirikisha wataalamu wanapokata miti mikubwa ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika mochari ya eneo hilo ukisubiri maandalizi ya mazishi.