Tottenham wanaongoza ligi kuu ya Uingereza Kwa alama ishirini na tatu baada ya kushinda mabao mawili dhidi ya Fulham hapo jana.Nahodha Son na Maddison ndio wafungaji wa mabao hayo.
Asenali nao wanajiandaa dhidi ya Sevilla usiku wa leo.Baada ya kutoka Sare ya mabao mawili dhidi ya Chelsea wikendi iliyopita,The Gunners wana Imani ya kupata ushindi siku ya Leo.Akimzungumzia Kai Havertz,Mikel Arteta ana imani na mchezaji huyo ligi ya mabingwa ikizingatiwa.Fabio Viera na Aaron Ramsdale wamekuwa kwenye mazoezi siku ya Leo.
Manchester United nao wako mbioni angalau kupata alama 3 dhidi ya Copenhagen siku ya Leo.Hawajapata matokeo bora ligi ya mabingwa ulipoanza.Mchezaji Casemiro amekua kwenye mazoezi pia bali hatocheza kwani anagharamikia Kadi nyekundu
Lens watachuana na PSV
Braga watawaalika Real Madrid
Benfica wakiwaalika Real Sociedad na mwishowe Union Berlin wakiwaalika Napoli.
Mechi za mapema ni kama
Galatasary wakiwaalika Bayern Munich
Intern Milan wakiwaalika RB Salzburg.
Na Michael Simiyu.