Kuendelea kupanda kwa thamani nya dola ya marekani kumeathiri pakubwa gharama ya kuendesha biashara nchini Kenya, pamoja na ununuzi wa bidhaa mbalimbali, leo gavana wa benki kuu nchini ;Kamau Thugge ,amefika katika bunge la kitaifa kujibu maswali mbele ya kamati ya fedha, Kamau ameanza kwa kutoa mwelekeo wa jinsi benki mbalimbali zinafaa kuendesha shughuli zao za kibiashara.
Gavana huyo wa benki kuu anasema mwaka huu kumekuwepo na ukuaji wa biashara katika benki za humu nchini, ikilinganishwa na mwaka jana tangu achukue majukumu ya kuwa gavana wa benki, Thugge amezitaka benki za kibinafsi kuwa mstari wa mbele kufanikisha biashara na uhusiano mwema wa kimataifa.
Kwa mujibu wa gavana wa benki kuu ni kwamba taifa la Kenya limejizatiti kuhakikisha linadumisha ubora wa sarafu yake ambayo imedumu kwa mda mrefu, Thugge anasema wanazidi kuvjtia wafadhili kufanikisha ukuaji wa biashara nchini.
Kwa sasa, kamataifa linatarajia kupata mkopo wa dola milioni mia nne, kutoka benki ya dunia IMF Thugge amepuuzilia mbali hataua ya iwapo wananchi watalalamika kuhusu ukopaji wa madeni unaofanywa na serikali ya rais William Ruto ikizingatiwa kua gharama ya maisha ni ghali kwa sasa.
Gavana huyo anasema kupanda kwa thamani ya dola ya marekani kunatokana na kuathirika kwa biashara baina ya benkiza humu nchini, amesema benki zilikuwa zimefeli kufanya biashara mwaka jana, kwa sasa anasema kuwa hali itaendelea kua shwari mda unaposonga.
Na Felix Wanjala