

Katika tukio la kusisimua, Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limemteua Benni Saul McCarthy, mwenye umri wa miaka 47, kama kocha mpya wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars. Uteuzi wa gwiji huyo wa soka kutoka Afrika Kusini unatarajiwa kuleta msisimko na matarajio mapya miongoni mwa mashabiki wa soka nchini.
Benni McCarthy amekuwa na taaluma maarufu katika soka, akicheza katika baadhi ya vilabu maarufu zaidi ulimwenguni. Kuanzia mwaka wa 1995 hadi 1997, McCarthy alichezea timu ya Seven Stars.McCarthy aliichezea timu ya taifa ya Afrika Kusini kutoka mwaka wa 1997 hadi 2012, akicheza mechi 79 na kufunga mabao 31. Baadaye, alichezea Celta Vigo nchini Uhispania, ambapo aling’ara kati ya mwaka wa 1999 hadi 2003. Mwaka wa 2003 hadi 2006, alijiunga na FC Porto nchini Ureno, kisha akahamia Blackburn Rovers nchini Uingereza kuanzia mwaka wa 2006 hadi 2010. Pia, nchini Uingereza, alijiunga na West Ham United kuanzia mwaka wa 2010 hadi 2011 kabla ya kwenda Orlando Pirates hadi mwaka wa 2013.

Mbali na taaluma yake ya vilabu, McCarthy aliichezea timu ya taifa ya Afrika Kusini kutoka mwaka wa 1997 hadi 2012, akicheza mechi 79 na kufunga mabao 31. Uzoefu mkubwa wa McCarthy kama mchezaji unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa Harambee Stars anapochukua jukumu hili jipya.