
BY FELIX WANJALA
Karata za uchaguzi wa 2027 zinapoendelea kupigwa nchini,eneo la Magharibi limeonekana kuwa kivutio kikubwa, kwa viongozi mbalimbali,wanaotazamia kuwania kiti Cha urais mwaka ujao.
Ujio wa Katibu Mkuu wa ODM Edwin Sifuna,katika siasa za kitaifa, zimeonekana kulemaza juhudi za Gavana Kenneth Lusaka,za kuhahakisha eneo Hilo linaweka kura zake,kwenye kapu Moja kwa manufaa ya rais William Ruto.Kundi la viongozi wachanga, limechipuka, na kudai wakati ni sasa kwa eneo Hilo,kuwania cheo Cha urais,Wala sii kumuunga mtu mwingine achaguliwe.
Kauli za viongozi hao zimeonekana kuwasimumua wapiga kura ambao wanadai eneo la Magharibi lina idadi kubwa ya wapiga kura na hivyo ni haki pia liunge mkono kiongozi mmoja wa eneo Hilo,kuongoza Taifa hili.
Lusaka ambaye hivi karibuni,aliteuliwa na rais William Ruto,kuwa mratibu mkuu wa kampeni za Kenya kwanza eneo Hilo, kwa kuelezea wananchi,kile ambacho serikali imefanya, na kile inapanga kufanya kwa manufaa ya maendeleo.Licha ya Lusaka kudai serikali ya Kenya kwanza imetunuku eneo la Magharibi,vyeo kadhaa kwenye Baraza la mawaziri,na jamii kuwa nambari tatu kitaifa,ufufuzi wa viwanda,ujenzi wa Barabara pamoja na masoko, Bado eneo Hilo linaonekana kuwa katika hali ya mapinduzi ya Kisiasa.
Miongo kadhaa iliyopita, eneo la Magharibi, lilikuwa na viongozi waliokuwa mstari wa mbele,kupigania haki ya mwananchi, pamoja na kuwa na tamaa ya kutaka kuongoza Taifa hili, miongoni mwao, Masinde Muliro,na Wamalwa Kijana.
Edwin Sifuna ameibuka kuwa,kati ya viongozi hao katika siasa za Sasa,huku viongozi mbalimbali wanaojihusisha naye,wakionekana kutoa onyo, kwa yeyote atampinga kuwa atapoteza umaarufu na cheo anachoshikilia.
Mabadiliko ya Kisiasa yakiendelea kushamiri eneo Hilo,ushindani mkali baina ya viongozi wanaoendesha siasa zilizopitwa na wakati,dhidi ya viongozi wanaopiga siasa za wakati wa Sasa huenda zikashika Kasi na hata matokeo kuanza kuonekana kabla na baada ya Uchaguzi mkuu ujao.Ubabe baina ya mtu wa mkono wa rais,Gavana Kenneth Lusaka dhidi ya Seneta Edwin Sifuna unaendelea kujitokeza mda unavyosonga, upande wa serikali unazidi kuelezea jinsi miradi mbalimbali ya mabilioni ya pesa imewekezwa eneo Hilo huku upande wa Sifuna ukidai ni lazima eneo Hilo lifanye mabadiliko ya uongozi.