Vijana Bungoma Wapaza Sauti.AI-Generated Image. TMG Stock
TANDAO MEDIA NEWS

Vijana na wasanii wa Kaunti ya Bungoma walijitokeza kwa wingi katika mkutano wa kuwawezesha vijana uliofanyika viwanja vya Uwanja wa Ndege, Kanduyi. Kauli yao kuu ilikuwa wazi: wanataka ushirikishwaji wa kweli, si ahadi za kila uchaguzi.
Maria Lucy alisema ni wakati viongozi waache siasa za picha na kuwekeza kwenye vipaji vya ndani. Msanii Ian Vishindo alisisitiza umuhimu wa inclusivity na msaada kwa wasanii wa ndani, akisema wengi wanakosa majukwaa na ufadhili. Joseph Wekesa wa Legacy Entertainment Group alieleza changamoto za ukosefu wa vifaa na matangazo, akisema msaada utainua Bungoma kitaifa. Miss Kisiwa alikemea upendeleo wa viongozi wanaowalenga vijana wachache kwa maslahi binafsi, akisisitiza usawa na nafasi sawa kwa wote.
Ian Dawood wa TV47 aliwahimiza vijana kutumia mitandao ya kijamii kukuza vipaji vyao, akimtaja Eric Nakhurenya kama mfano wa kuunga mkono vijana wa eneo hilo.
Seneta alitangaza nia ya kuwania kiti cha Seneta mwaka 2027, akiahidi kushirikiana na vijana mapema bila kusubiri kuchaguliwa. “Sitasubiri kuchaguliwa ndio niwasikilize. Tuanze sasa,” alisema.Mkutano huo ulionyesha msimamo wa vijana wa Bungoma: wanataka fursa, msaada wa kweli, na nafasi ya kushiriki moja kwa moja katika maamuzi ya maendeleo.
