Maumivu katika kipindi cha hedhi kwa mwanamke ni dalili ya hali ya endometriosis.Wataalam wa afya
wamebainisha hali hii ambayo huathiri wanawake hasa wa kati ya umri wa miaka 15 – 44.
Hali ya endometriosis yaweza kuenea nje ya kizazi huku ikiathiri viuongo kama tumbo , shingo ya uzazi
na hata kibofu. Hata hivyo kaunti ya Nairobi inashughulikia hali hii kwa njia ya matibabu ya upasuaji .
Takriban wanawake milioni 200 duniani wameathirika na hali hii duniani ,ilhali Kenya haina data sahihi
ambayo husababishwa na hali ya unyanyapaa na kukosa kugundua usahihi wa hali hii.Baadhi ya dalili za
ugonjwa huu ni maumivu katika tumbo la chini , hedhi nzito , maumivu wakati wa haja ndogo, maumivu
wakati wa tendo na ndoa na kutokwa na ndoa.
Nairobi imethibitisha kituo cha kutibu hali hii huku wataalam wa afya wakishughulikia matibabu
hata hivyo ,wametoa wito kwa serikali kuhusisha hali ya endometriosis katika mpango mzima wa UHC
kwa kugharamia matibabu haya kwani upasuaji wa hali ni marufuku hivyo kuwaacha wanawake wengi
kwa machungu.
na Abigaely Wanjala