
BY FELIX WANJALA
Utafiti wa shirika la infotrak uliofanywa tarehe 29 mwezi desemba mwaka wa 2025,uliangazia umaarufu wa baadhi ya viongozi eneo pana la Magharibi.Watu 600 walifanyiwa mahojiano katika Kaunti 5 za eneo Hilo ukiwa ni pamoja na Vihiga,Busia, kakamega,Transnzoia na Bungoma,waliohojiwa walikuwa kati ya miaka 18 na zaidi na wengi wao wakiwa wamesajiliwa kama wapiga kura.
Katika utafiti huo rais William Ruto ndio chaguo la wengi eneo Hilo kama mgombea wa kiti Cha urais kwa aslimia 25, Naibu kiongozi wa chama Cha jubilee Fread Matiang’i aliibuka wa pili kwa aslimia 15,huku Gavana wa Kaunti ya Transnzoia George Natembeya akipata aslimia 13.Utafiti huo pia uliangazia umaarufu wa vyama vya kisiasa huku chama Cha ODM kikiongoza kwa aslimia 25,chama tawala Cha UDA kikipata aslmia 20 huku kike Cha DCP kikipata aslmia 7.

Kwenye ulingo wa Kisiasa,eneo Hilo Gavana George Natembeya alionekana kuendelea kama kiongozi wa eneo Hilo kwa aslimia 50%, Mkuu wa Mawaziri Musalia Mdavadi akifuata kwa aslimia 32% Huku Katibu Mkuu wa chama Cha ODM Edwin Sifuna akipata aslimia 31%,spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula akishikilia nafasi ya nne kwa aslimia 29% Wycliffe oparanya alipata 14% huku Eugene Wamalwa akipata 13%.Ubabe wa Kisiasa umekuwa ukishuhudiwa eneo Hilo huku viongozi mbalimbali walionyesha nia ya kuongoza jamii ya Mulembe.