Kenya's opposition party National Super Alliance (NASA) leader Raila Odinga looks at supporters after giving a speech at Ruaraka in Nairobi, on November 19, 2017. - Four bodies were discovered on November 19, a day before Kenya's Supreme Court was to rule on whether current President can be sworn in for a second term or if there must be another re-run. (Photo by YASUYOSHI CHIBA / AFP) (Photo by YASUYOSHI CHIBA/AFP via Getty Images)

BY FELIX WANJALA.
Chama cha ODM kinaendelea kukumbwa na changamoto za kisiasa baada ya kufariki kwa kiongozi wake wa muda mrefu, Hayati Raila Odinga, hali inayozua maswali kuhusu mustakabali wa chama hicho katika siasa za kitaifa.Baadhi ya wananchi wamekumbusha kuwa ODM ina katiba inayopaswa kuzingatiwa na viongozi wake wanapotekeleza majukumu ya chama, wakisisitiza umuhimu wa uongozi wa kisheria na uwajibikaji.
Katika mjadala mpana kuhusu mwelekeo wa ODM, maoni yamegawanyika,wengine wakihimiza ushirikiano na serikali ya Rais William Ruto, huku wengine wakikitaka chama kujiimarisha kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2027.Hata hivyo, katika mkutano wa viongozi wakuu wa ODM uliofanyika jijini Nairobi, chama kiliafikia uamuzi wa kushirikiana na serikali ya Ruto kwa masharti kwamba ajenda kumi zilizokubaliwa zitatekelezwa kikamilifu kabla ya mwaka wa uchaguzi wa 2027.
Uamuzi huo unaashiria mwelekeo mpya wa ODM katika enzi ya baada ya Raila, huku chama kikitafuta njia ya kudumisha ushawishi wake wa kisiasa na kuendeleza ajenda za maendeleo kwa taifa.