 
                President William with Kanu national chairman Gideon Moi at State House on October 8, 2025. /PCS

BY FELIX WANJALA.
Siku chache baada ya kuanzisha ushirikiano wa kisiasa na kiongozi wa KANU Gideon Moi, Rais William Ruto ametua katika ngome ya Moi huko Baringo kwa ziara ya maendeleo iliyojaa ishara za kisiasa.Katika ziara hiyo, Rais Ruto alimpigia debe mgombea wa useneta kwa tiketi ya UDA, akisisitiza kuwa ushirikiano wake na Moi ni hatua ya kuunganisha taifa kwa ajili ya maendeleo ya pamoja.
“Tunataka siasa za mshikamano na maendeleo, si za migawanyiko,” alisema Rais.Rais alitangaza miradi kadhaa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, nyumba za bei nafuu, na kufutwa kwa ada ya kutafuta vitambulisho hatua iliyopokelewa kwa shangwe na wananchi wa Baringo.
Wakati huo huo, katika Kaunti ya Kakamega, eneo la Malava, kikosi cha DAP-K kikiongozwa na Gavana wa Trans Nzoia George Natembeya kilifanya mkutano wa kisiasa ambapo Natembeya alimsuta msaidizi wa Rais, Farouk Kibet, kwa madai ya kuikosea heshima jamii ya Mulembe.
Lakini Seneta wa Kakamega Boni Khalwale aligeuza mkutano huo kuwa jukwaa la kumpigia debe mgombea wa ubunge wa DAP, Seth Panyako, akisisitiza umuhimu wa uongozi wa kitaifa unaojali maslahi ya wananchi.

 
                 
                 
                 
                 
                 
                